1 Thessalonians 4:1-6

Maisha Yanayompendeza Mungu

1 aHatimaye, ndugu, tuliwaomba na kuwasihi katika Bwana Isa kwamba, kama mlivyojifunza kutoka kwetu jinsi iwapasavyo kuishi ili kumpendeza Mungu, kama vile mnavyoishi, imewapasa mzidi sana kufanya hivyo. 2Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa mamlaka ya Bwana Isa.

3 bMapenzi ya Mungu ni kwamba ninyi mtakaswe, ili kwamba mjiepushe na zinaa, 4 cili kwamba kila mmoja wenu ajifunze kuutawala mwili wake mwenyewe katika utakatifu na heshima, 5 dsi kwa tamaa mbaya kama watu wa Mataifa wasiomjua Mungu. 6 eKatika jambo hili mtu asimkosee ndugu yake wala kumlaghai. Kwa kuwa Bwana ni mlipiza kisasi katika mambo haya yote, kama vile tulivyokwisha kuwaambia mapema na kuwaonya vikali.
Copyright information for SwhKC